FAIR LAB

Jumapili, 11 Agosti 2013

AJALI YA GARI LA TANESCO IMETOKEA USIKU HUU KWA SADALA MOSHI...

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
Gari la shirika la umeme Tanzania (Tanesco) imepinduka usiku huu baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corola katika eneo la Kwa Sadala barabara ya Moshi/Arusha.
Kwa mujubu wa shuhuda wa ajali hiyo, gari la Tanesco lilikuwa limepakia wafanyakazi wa shirika hilo wapatao 18 wakitokea eneo la KIA kuelekea mjini Moshi.
Amesema dereva wa gari dogo alikuwa akijaribu kuzipita gari kadhaa zilizokuwa zikielekea Arusha ndipo akakutana na Loli hilo kabla ya kurudi upande wake.
Ndipo gari magari hayo yakagongana na kisha gari la Tanesco kupinduka. Shuhuda amesema majerhi wa ajali hiyo walikimbizwa hosptali ya KCMC huku dereva wa gari hilo dogo akiingia mitini na kutokomea kusiko julikana.

Toyota Corola lililosababisha ajali hii


Askari wa usalama barabarani na gari la tanesco lililopinduka

Wadau eneo la tukio

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni